Uongozi wa azam fc wamekana tafiti hiyo iliyowekwa katika blogu ya shaffihdauda.com ikiwa na anuwani www.shaffihdauda.com/2013/03/madudu-ya-ligi-kuu-mechi-zinaonyeshwa.html
"Mechi za VPL zinaooneshwa kwa udhamini wa SSB zimekuwa za dhuluma kuwa ni uongo na uzushi," ilieleza taarifa iliyowekwa na meneja wa Azam fc Patrick Kahemele katika ukurasa wa azam ndani ya facebook.
Kahemele alieleza kuwa JKT Ruvu inayohusishwa katika tafiti hiyo na kudai kuwa haijalipwa, anasema kuwa teyari wameshailipa na wako mbioni kuwalipa Polisi morogoro.
"Klabu ya JKT Ruvu iliyotajwa kuwa imelalamika ilipokea malipo toka kwa star tv yaliyolipwa na azam fc kwa niaba yake, pia malipo ya Polisi moro yanaandaliwa na yatafanyika wiki ijayo," ilieleza taarifa ya Kahemele.
Kahemele alihitimisha taarifa yake kwa kuwaomba wananchi waipuuze tafiti hiyo;
"Tunawaomba wananchi waipuuze habari hiyo kwa kuwa ni uzushi".
--
MSUNI COMPUTER SOLUTION
NDIO SULUHISHO LA TATIZO YA COMPUTER YAKO
+255-657-148-283 (Habib)
+255-657-184-421 (Msuni)
www.aboodmsuni21.blogspot.com
0 Maoni:
Post a Comment