Azam fc leo waliwakaribisha Prinsons katika uwanja wake wa azam complexs katika muendelezo wa michezo ya ligi kuu ya vodacom uliomalizika kwa azam fc kuibuka na ushindi wa goli 3-0.
Prinsons waliuwanza mchezo wa leo vyema kwa kuwazuia azam fc kutopata goli la mapema lakini walitepeta katika dakika ya 19 kufuatia kazi nzuri ya kiungo Khamis Mcha aliyemtengea Kipre Tchetche na bila kufanya agizi Tchetche aliiandikia goli la kwanza azam fc.
Kuingia kwa goli hilo kulipelekea Prisons kurejea nyuma na kupeleka mashambulizi ya kushtukiza ambayo yalikuwa yanaishia kwa kipa Mwadini Ally na kupelekea kwenda mapumziko wakiwa nyuma kwa goli 1-0.
Azam fc walirejea kipindi cha pili na kucheza kwa tahadhari kubwa uku wakiendelea kutawala mchezo na mnamo dakika 75 John Raphael Bocco aliiandika azam fc goli la pili kwa shuti kali akitokea pembeni.
Azam fc walimpumzisha Khamisi Mcha, Humphrey Mieno na Salum Aboubakary na nafasi zao kujazwa na Abdallah Seif, Abdi Kassim na Ibrahim Mwaipopo, mabadiliko yaliyoendeleza mchezo kuwa chini ya azam fc.
Katika dakika ya 85 alikuwa Kipre Tchetche aliyeizawadia azam fc goli la la 3 na kupelekea mchezo kumalizika kwa azam kushinda 3-0.
Azam fc leo: MWADINI ALLY, HIMID MAO, WAZIRI SALUM, JOACKINS ATUDO, LACKSON KAKOLAKI, MICHAEL BOLOU, KIPRE TCHETCHE, SALUM ABOUBAKARY /IBRAHIM MWAIPOPO, JOHN BOCCO, HUMPHREY MIENO/ ABDI KASIM NA KHAMISI MCHA/ ABDALLAH SEIF
kipre tchetche 18, 85, john bocco 75
--
MSUNI COMPUTER SOLUTION (Tunarejesha uhai wa computer)
www.aboodmsuni21.blogspot.com/p/msuni-computer-solution_7934.html
[+255 657 184 421]
0 Maoni:
Post a Comment