Sunday, March 17, 2013

VIJANA WA UNGUJA WAMUINAMISHA KICHWA RAISI WA LIBERIA

Posted By: kj - 9:27 PM

Share

& Comment

Vijana wa unguja wanaokipiga katika timu ya azam fc Khamisi Mcha na Abdallah Seif wamemtoa raisi wa Liberia kichwa chini baada ya kuiwezesha azam fc kuichapa timu ya mtoto wa raisi huyo barrack YC II goli 2-1.

Azam fc wameibuka na ushindi huo wa guli 2-1 mbele ya wengeji wao Barrack YC ukiwa mchezo wa kombe la shirikisho uliochezwa katika jiji la Monirivo nchini Liberia na kuhudhuriwa na raisi wa nchi hiyo.

Azam fc waliuwanza mchezo huo kwa kasi na kuutawala mchezo huo kwa dakika 40, za kipindi cha kwanza. Katika dakika 20 za mwanzo zilimalizika bila ya kipa wa azam fc Mwadini Ally kudaka mpira wowote ule huku washambuliaji wa azam waliokuwa wanaongozwa na nahodha John Bocco wa kishindwa kuipatia azam goli la kuongoza.

Katika kipindi cha kwanza Barrack YC II walitengeneza nafasi 3 na kufanikiwa kuitumia vyema nafasi moja kupitia kwa Joal Dauda alipoipatia barrack YC II goli la kuongoza katika dakika ya 45 na kupelekea ubao kusomeka goli 1-0 wakati wanakwenda mapumziko.

Azam fc walirejea kwa kasi katika kipindi cha pili huku Barrack YC II wakitaka kulinda goli lao 1, alikuwa Humphrey Mieno aliye utegua mtego wa kuotea na kuisawazishia azam katika dakika ya 55.

Baada ya kuingia goli hilo kocha wa azam Stewart Hall aliwapumzisha Ibrahim Mwaipopo, Kipre Tchetche na John Bocco na nafasi zao kuchukuliwa na Abdi Kassim, Abdallah Seif na Jabir Azizi.

Mabadiliko hayo yalizaa matunda baada ya Khamisi Mcha kumtengenezea nafasi Abdallah Seif ya kufunga goli la pili na bila ajizi Seif alimalizia kazi nzuri ya Mcha na kuiandikia azam goli la pili katika dakika ya 90 na kupelekea mchezo kwisha kwa matokeo 2-1.

kikosi kazi cha azam kinataraji kuanza safari kesho saa 11 jioni kwa saa za Liberia ya kurejea nyumbani ambapo wanataraji kutua nchini saa 2 asubuhi kesho kutwa.

kikosi kilicho cheza leo:
MWADINI ALLY
HIMID MAO
WAZIRI SALUM
DAVID MWANTIKA
JOACKINS ATUDO
MICHAEL BOLOU
KIPRE TCHETCHE/ABDALLAH SEIF
IBRAHIM MWAIPOPO/ABDI KASSIM
JOHN BOCCO/JABIR AZIZI
HUMPHREY MIENO
KHAMISI MCHA


--
MSUNI COMPUTER SOLUTION
NDIO SULUHISHO LA TATIZO YA COMPUTER YAKO
+255-657-148-283 (Habib)
+255-657-184-421 (Msuni)
www.aboodmsuni21.blogspot.com

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.