Friday, April 26, 2013

AZAM KUSAKA MAKALI KWA COASTAL LEO

Posted By: Unknown - 6:25 AM

Share

& Comment

Wawakilishi wa Tanzania katika michuano inayoandaliwa na shirikisho la soka la Africa 'CAF' Azam FC leo itakuwa katika uwanja wa Mkwakwani wakiwakabili Coastal union kabla ya kusafiri kwenda Moroco kuwavaa AS FAR RABAT.

Azam na Coastal union wanakutana katika muendelezo wa michezo ya ligi kuu ya vodacom, ambapo kwa leo kutakuwa na mchezo mmoja tu.

Azam wanaitaji ushindi katika mchezo wa leo ili kuzidi kujikita katika nafasi ya pili ya msimamo wa ligi huku wakiendelea kuuchelewesha ubingwa kwenda yanga wanaosaka point moja katika michezo miwili walio salia nao.

Azam fc leo huenda watakosa huduma ya beki toka Kenya Jackson Atudo aliyeumia katika mchezo awali wa raundi ya tatu wa kombe la shirikisho dhidi ya AS FAR Rabat sambamba na beki Samih Hajji Nuhu.

Kwa mara kadhaa azam fc wamekuwa wakiwafunga Coastal union wanapokutana katika michuano mbalimbali.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.