Friday, April 26, 2013

MSAFARA WA WATU 55 KWENDA MOROCO

Posted By: azam fans - 6:53 AM

Share

& Comment

Msafara wa azam fc kwenda nchini Morocco kwa ajili ya mchezo wa marejeano wa kombe la shirikisho dhidi ya AS FAR Rabat unatarajiwa kuwa na jumla ya watu 55, ambao utaondoka jumapili ya aprili 28.

Katika msafara huo utawajumuisha wachezaji wote waliosajiliwa kwa ajili ya michuano hiyo ukiwaondoa Samih Hajji Nuhu aliyemajeruhi na kiungo Abdulhalim Homoud aliyejiunga na Cosmos ya Afrika kusini.

Vile vile benchi lote la ufundi linaloongozwa na Muingeleza Stewart Hall utakuwa miongoni mwa sehemu ya msafara huo.

Hata hivyo uongozi wa azam fc teyari wameshatanguliza watu nchini Moroco kwa ajili ya kuweka mazingira sawa yatakayo fikiwa na kikosi chao.

Azam fc katika mchezo huo utakao chezwa mei 5 mwaka huu wanatakiwa kutoka na ushindi ama sare ya magoli kufuatia mchezo wa awali kwisha kwa sare ya bila kufungana.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.