Monday, December 23, 2013

MSHAMBULIAJI MPYA WA AZAM FC KUANZA KUONEKANA DES 26 DHIDI YA SHOOTING

Posted By: kj - 7:03 AM

Share

& Comment

Ismail Mohammed Kone katika moja ya mazoezi ya Azam fc
Katika kuimmarisha kikosi cha mabingwa wa kombe la mapinduzi Azam FC wameongeza nguvu katika upande wa ushambuliaji baada ya kummsajili mshambuliaji toka Ivortcoast Ismail Mohammed Kone.

Kone aliyejiunga na Azam FC kutoka katika timu ya Stella Abidjan ya Ivory Coast, anatarjiwa kuiwakilisha Azam FC katika michuano ya Mapinduzi CUp inayoanza januari mosi mwakani kabla ya kuonekana katika ligi kuu ya TAnzania BAra hapo januari 25 mwakani.

Kone huenda akaonekana katika mchezo wa kirafiki utakao tumiwa na shirikisho la soka nchini (TFF) kupima mfumo mpya wa tik
eti za kuingilia viwanjani ambapo Azam FC itakapo menyana na Ruvu shooting katika uwanja wa Azam complexs uliopo Chamanzi jijini Dar es salaam hapo desember 26 mwaka huu.

Kone aliyesajiliwa na Azam FC kukamilisha idadi ya wachezaji wa tano wa kimataifa wa Azam FC baada ya beki kutoka Kenya Joackins Atudo kumaliza mda wake wa kuitumikia Azam FC na kutengeneza nafasi ya mshambuliaji huyo toka Ivory coast.


Kone anungana na wechezaji wenzake wa wawili kuroka Ivory coast mapacha Kipre Tcheche na Kipre Bolue na kuifanya Azam FC kuwa na wachezaji watattu kutoka katika taifa hilo linaloongoza kwa soka barani Afrika kwa mujibu wa takwimu za FIFA.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.