Saturday, December 7, 2013

OMOG AREJEA CAMEROON KUMALIZIA LIKIZO

Posted By: Unknown - 2:09 PM

Share

& Comment


Na Azam FC
Joseph Marius Omog, Kocha mkuu wa Azam FC amesafiri kurudi nchini Cameroon kumalizia likizo yake ambako atakaa kwa muda wa wiki mbili kabla ya kurejea nchini tarehe 20 December kuendelea na majukumu yake.

  Kocha Omog amekuwa kwenye majukumu ya kazi tangia January 2013 na timu ya AC Leopards ambapo alimaliza majukumu yake Novemba 24 kwa kutwaa vikombe vya FA na Ligi kuu kisha kurudi nchini Cameroon kukaa siku nne tuu kabla ya kuja nchini ku-sign mkataba wa kuifundisha Azam FC

Kabla ya kuondoka kocha ameacha program ya wiki mbili kwa wasaidizi wake Kally Ongala na Ibrahim Shikanda ambao wanapewa sapoti na na kocha wa Under 20 Vivek Nagul

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.