Sunday, February 16, 2014

LIVE AZAM TV: Ferroviario vs Azam FC Beira leo

Posted By: Unknown - 10:24 AM

Share

& Comment

https://fbcdn-photos-g-a.akamaihd.net/hphotos-ak-frc3/t1/p600x600/1925123_705274796179546_1589327635_n.jpg
Na Florian Kaijage, Beira

Habari za asubuhi wadau wa Azam TV, usikose kufuatilia kitakachokuwa kinajiri hapa Beira katika pambano la marudiano la kombe la Shirikisho Afrika kati ya wenyeji Ferroviario (Reli) da Beira na Wawakilishi wa Tanzania Azam.

Kumbuka mtanange umepangwa kupigwa kuanzia saa 9 alasiri za hapa Msumbiji sawa na saa 10 za nyumbani Afrika Mashariki.

Jambo lingine muhimu la kufahamu ni kuwa timu imefika hapa Jumatano usiku ni Jumamosi tu jua lilitoka na mvua haikunyesha kabisa.

Lakini leo tangu alfajiri mvua kubwa imekuwa ikinyesha na anga limetanda mawingu mazito; dalili kuwa mvua itaendelea kunysha kwa muda mrefu kutwa ya leo.

Kwa muda wote Azam imekuwa ikifanya mazoezi katika viwanja vilivyojaa maji. Mara ya mwisho kufanya mazoezi katika uwanja utakaotumika kwa mchezo leo ilikuwa Ijumaa alasiri na sehemu kubwa ya uwanja ilikuwa imejaa maji.

Kwa mujibu wa Kanuni za CAF (Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika) zinazoendesha mashindano ya Kombe la Shirikisho, mchezo wowote ambao haukumalizika kutokana na hali mbaya ya uwanja (pitch) au hali mbaya ya hewa, utachezwa ndani ya saa 24 baadaye.

Kanuni ya 7(7)inasomeka "Ikiwa mchezo utasitishwa kabla ya muda wa mchezo kumalizika kwa sababu zilizo nje ya uwezo hususan kwa sababu ya hali mbaya ya uwanja na/au hali mbaya ya hewa kwa uamuzi wa mwamuzi, mchezo huo utachezwa saa 24 baadaye katika uwanja uleule na waamuzi walewale. Hatua zote za kinidhamu (kadi za njano na nyekundu) zilizochukuliwa wakati wa mchezo uliovunjika zitabakia kwa mujibu wa Kanuni ya adhabu ya CAF".

Suala la mvua na hali ya uwanja lilijitokeza na kujadiliwa wakati wa kikao cha matayarisho ya mchezo kilichofanyika jana katika Hoteli ya Tivoli hapa Beira.

Kamishna wa mchezo wa leo Charles Kafatia kutoka Malawi aliwaambia wawkilishi wa klabu mbili na waamuzi kutoka Zambia wakiongozwa na Wisdom Chewe kuwa iwapo uwanja utaendelea kuwa katika hali isiyoridhisha basi kanuni zitafuatwa na mwasiliano kupelekwa CAF.

Kwa mujibu wa ratiba ya kiutawala, Kamishna Kafatia akifutana na mwamuzi wa akiba atakwenda uwanjani saa 4 asubuhi hii kukagua masuala muhimu ikiwepo sehemu ya kuchezea na taratibu za kiusalama.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.