Omog amesema hayo baada ya mchezo wa kirafiki uliochezwa hii leo katika uwanja wa Azam copmlex uliomalizika kwa sare ya goli 1-1, ambapo Azam FC walikuwa wanapimana ubavu na Polisi Morogoro.
Omog amesema katika michezo hiyo ya kirafiki haangalii zaidi Matokeo yanayopatikana Bali kikubwa anachoangalia mapungufu ambayo yanaonekana kwa wachezaji wake ili kuweza kuyafanyia kazi kabla ligi kuu Kuanza.
Katika mchezo wa leo goli la Azam FC lilifungwa na Lionel Saint-preux huku la Polisi Morogoro likifungwa na Danny Mrwanda aliyekuwa anakipiga Vietinam kabla ya kurejea nchini na kujiunga na Polisi Morogoro..
Huo unakuwa mchezo wa kwanza katika mechi za kujiandaa na msimu Azam inashindwa kuondoka na ushindi, baada ya awali kuzifunga 1-0 Ruvu Shooting, 2-1 Friends Rangers, 3-2 kombaini ya Jeshi, 1-0 Polisi Morogoro na 2-1 JKT Ruvu.
Kikosi cha Azam kinakwenda mapumziko ya sikukuu ya Eid El Fitri na kinatarajiwa kurudi mazoezini kuanzia Jumatano wiki ijayo.
PICHA NA BIN ZUBEIRY ZA MICHEZO WA LEO
Kipre Balou akiwakimbiza viungo wa Polisi, huku kaka yake Kipre Tchetche akiwa tayari kumsaidia |
Kipre Balou akifanya vitu adimu pembeni ya wachezaji wa Moro |
David Mwantika akikosa bao la wazi baada ya kupanda kusaidia mashambulizi |
Kipre Tchetche akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Polisi |
Didier Kavumbangu akimiliki mpira mbele ya beki wa Polisi |
Gaudence Mwaikimba akimiliki mpira mbele ya beki wa Polisi |
0 Maoni:
Post a Comment