Sunday, August 31, 2014

AZAM FC KUINGIA MKATABA NA NMB

Posted By: Unknown - 9:31 PM

Share

& Comment

http://24tanzania.com/wp-content/uploads/2013/05/844bAzam-FC5.jpg
Mabingwa wa soka nchini Azam FC wanatarajia kuingia mkataba wa udhamini na benki ya NMB siku ya jumatano wiki hii.

Msemaji wa Azam FC Japhari Iddi Maganga akiwa anaongea na sports extra hii leo amesema kuwa NMB wanataraji kuingia mkataba na Azam FC ambapo mambo yatawekwa hadharani siku ya jumatano wiki hii.

Maganga alisema kuwa kila kitu kinaenda sawa na taratibu za mkataba huo wa udhamini zilianza mda mwingi uliopita na siku ya jumatano kila kitu kitawekwa hadharani.

NMB inatarajiwa kuwa mdhamini wa kwanza wa Azam FC kutoka nnje ya bidhaa za kampuni ya Said Salim Bakharesa wanao miliki timu hiyo ya Azam FC.

Maganga akizungumzia maandalizi ya ligi kuu na mchezo wa ngao ya jamii alisema kuwa wachezaji wameshaanza mazoezi toka alhami isipokuwa kwa wale wachezaji walioitwa kwenye timu ya taifa kwa ajli ya mchezo wa kirafiki.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.