Thursday, August 28, 2014

DUMAYO KUREJEA JANUARI, KIMWAGA MACHI

Posted By: Unknown - 7:21 PM

Share

& Comment

DAKTARI wa Azam, Mwanandi Mwankenwa, amethibitisha kuwa kiungo Frank Domayo na Joseph Kimwaga wa Azam watarejea kwenye Ligi Kuu Bara mwanzoni mwa mwaka 2015.
Mwankenwa amelieleza Mwanaspoti kuwa Domayo ambaye alisainiwa akitokea Yanga atakuwa fiti kucheza michezo ya ligi kuanzia Januari Mosi wakati Kimwaga atasubiri hadi Machi Mosi. Wachezaji hao wameanza mazoezi ya viungo kwenye hospitali ya ‘Sanitas Mikocheni Clinic’ iliyopo jijini Dar es Salaam.

“Kutokana na utaratibu wa matibabu walioelekezwa na madaktari bingwa wa mifupa waliowatibu, Domayo ataruhusiwa rasmi kucheza mpira wa kishindani ifikapo Januari Mosi 2015, kwa upande wa Kimwaga atachukua muda zaidi ya miezi miwili mbele mpaka Machi,”alisema Daktari huyo.
Kwa mujibu wa ratiba ya ligi kuu 2014/15, Domayo ataweza kucheza michezo yote ya ligi kuu mzunguko wa pili na hata ile ya mashindano ya kimataifa. Kimwaga naye atarudi uwanjani mwezi machi na kucheza michezo saba ya ligi ambayo ni dhidi ya Coastal, Yanga, Mtibwa, Kagera, Stand United, Simba na Mgambo JKT.


CHANZO: MWANASAPOTI

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.