Safari ya Azam FC ya kutwaa ubingwa kwa mara ya kwanza ya kombe la Kagame imefikia Tamati hii leo baada ya kutolewa kwa mikwaju ya pentai 4-3 na El Merekh ya Sudan katika mchezo wa robo fainali ulio malizika hivi punde.
Katika mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Nyamirambo jijini Kigali Rwanda ulishuhudia dakika 90 zikimalizika kwa sare ya bila kufungana na changamoto ya mikwaju ya penati ikachukuwa hatima yake ya kuamua nani wa kusonga mbele.
Mchezo huo wa leo ulimshuhudia nahodha wa Azam FC John Raphael Bocco akishindwa kumalizia mchezo baada ya kuumia goti na nafasi yake kuchukuliwa na Didier Kavumbagu.
Katika kipindi cha kwanza Azam FC amanusura waandike goli la kuongoza baada ya kazi nzuri ya John Bocco kumkosa wa kumalizia, na kupeleka mchezo kwenda mapumziko ukiwa sare ya bila kufungana.
Shukrani zimuendee kipa Mwadini Ally Mwadini baada ya kufanya kazi nzuri katika dakika 20 za mwisho wa kipindi cha pili ambapo amanusura El Merekh waumalize mchezo katika dakika 90.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Maoni:
Post a Comment