Friday, August 22, 2014

JEMEDARI: HATUKUWA NA BAHATI

Posted By: Unknown - 5:14 AM

Share

& Comment


http://ptblog.pesatimes.com/wp-content/uploads/2014/04/jeme.jpg

BAADA ya kutolewa katika Kombe la Kagame, Meneja wa timu ya Azam FC, Jemedari Said, amesema timu yao ilikosa bahati na kujikuta ikitolewa mapema kinyume cha matarajio yao.

Mabingwa hao wa Tanzania Bara walitolewa katika robo fainali juzi dhidi ya El Merreikh kwa penalti 4-3 baada ya kumaliza dakika 90 bila kufungana mjini Kigali, Rwanda.

“Tulicheza vizuri karibu mechi zote kuanzia hatua ya makundi hadi ile ya robo fainali. Tulitengeneza nafasi nyingi, lakini tulikosa bahati kwa sababu tulishindwa kuzitumia ipasavyo,” alisema Said kwa simu jana.

“Lakini pamoja na kutolewa naamini tumepata mazoezi mazuri ambayo yatatusaidia katika ligi ya Vodacom.”

Alisema lengo lao lilikuwa na kurudi na taji hilo nchini ili kuendelea kujiwekea rekodi, lakini lengo lao halikutimia na kwa sasa wanajipanga kwa ajili ya kuhakikisha timu hiyo inaanza kwa kishindo mechi za Ligi Kuu mwezi ujao.

“Wakati tunakuja kushiriki mashindano haya lengo letu namba moja ilikuwa ubingwa na kingine ilikuwa ni kutumia mechi hizi kama maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu, ukizingatia siye ndiyo mabingwa watetezi. “Sasa tumekosa ubingwa langu tumepata mazoezi ambayo naamini yatakuwa na msaada kwetu,” alisema Said.

Azam FC ilishiriki Kombe la Kagame mwaka huu baada ya Yanga kufukuzwa kutokana na kupeleka kikosi cha wachezaji chipukizi. Kikosi cha Azam FC kinatarajia kuwasili Dar es Salaam kesho mchana ambapo wachezaji watapewa mapumziko ya siku mbili.

Baada ya hapo, wataingia kambini kuanza kujiandaa na mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga ambayo itachezwa kwenye Uwanja wa Taifa Septemba 13, kuashiria mwanzo wa msimu mpya wa Ligi Kuu Bara unaoanza Septemba 20.


CHAZNO: HABARI LEO

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.