Na Mahmoud Zubeiry, KIGALI
BEKI
Shomary Kapombe na mshambuliaji Lionel Saint- Preux kutoka Haiti wote
wamefanya mazoezi kikamilifu jana na leo kuelekea mchezo wa kesho wa
Robo Fainali Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame Azam
FC ikimenyana na El Marreikh ya Sudan, Uwanja wa Nyamirambo, Kigali,
Rwanda.
Wawili
hao waliokuwa wanasumbuliwa na maumivu ya nyama za paja, walikoa mchezo
wa mwisho wa Kundi A dhidi ya Adama City ya Ethiopia, Azam FC ikishinda
4-1.
Shomary Kapombe katikati (jezi namba nne) akifanya mazoezi kikamilifu na wenzake leo Uwanja wa Kiyovu, Nyamirambo |
Azam FC itamenyana na Merreikh kesho Uwanja wa Nyamirambo mjini Kigali |
Na
katika mazoezi ya leo asubuhi Uwanja wa Kiyovu, Nyamirambo mjini hapa,
kocha Mcameroon Joseph Marious Omog ameonekana kuwahusisha nyota hao
katika kikosi kitakachoanza kesho.
Majeruhi
mwingine, beki Waziri Salum pia amefanya mazoezi wakati kiungo Himid
Mao anatarajiwa kurudi pia baada ya kukosa mchezo dhidi ya Adama kwa
sababu ya kadi za njano.
Omog
amekuwa akiandaa Azam FC kitaalamu mno kuelekea mchezo huo,
akiwaelekeza mifumo na aina tofauti ya uchezaji, ikiwa ni pamoja na
kutumia mipira mirefu na mifupi.
Amekuwa
akiwandaa pia kwa kupiga penalti, kwa kuwa iwapo mchezo huo utamalizika
kwa sare, matuta yataamua timu ya kusonga Nusu Fainali.
Kwa
ujumla Azam ambayo imewekwa hoteli moja na wapinzani wao hao, Merreikh,
Kigali View eneo la Nyamirambo, ipo vizuri kuelekea mchezo huo, ambao
unasubiriwa kwa hamu na Watanzania wengi.
Robo
Fainali za Kagame zinaanza leo, mchezo wa kwanza ukiwa kati ya Polisi
ya hapa dhidi ya Atleitco ya Burundi, kabla ya Rayon Sport kumenyana na
APR, zote za hapa leo, wakati mbali na Azam na Merreikh, mchezo mwingine
wa kesho utakuwa kati ya KCC ya Uganda na Atlabara ya Sudan Kusini.
chanzo: bin zubeiry
0 Maoni:
Post a Comment