Sunday, August 17, 2014

AZAM KUWAKABILI EL MEREKH JUMATANO, ROBO FAINALI KAGAME CUP

Posted By: kj - 12:14 PM

Share

& Comment

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEim3VXQWwHquFESZinMmA8ZRWx8ajoHT-dQj0_rpAOwNKfV7EMtOS2h-QAvL4DKBS10PcotfshGjSDYEkUxkKXGp4TZM4a8HywDJhyphenhyphen1MUxBvJvxvw0seABQxau456Zcre78WIZIKVRIwwYr/s1600/8.jpg
 AZAM FC sasa itakutana na El Merreikh ya Sudan katika hatua ya robo Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, Jumatano katika Uwanja wa Nyamirambo mjini Kigali.
 

Azam FC itakutana na El mereikh baada ya kumaliza wa pili nyuma ya Rayon Sport iliyojikusanyia pointi 10 huku Azam FC ikikusanya pointi 8 katika kundi hilo la B.

Katika hatua ya makundi Azam FC imfanikiwa kutikisa nyavu za wapinzani mara 10 ikiwa ni mara nyingi kuliko timu nyinginezo zinazo shiriki michuano hiyo.


Magoli 10 ya Azam FC yamefungwa na wachezaji 6 tofauti huku mfungaji bora wa wakati wote John Bocco akiwa kinara wa mabao katika michuano hii, aiwa na jumla ya magoli matatu, huku Didier Kavumbagu na mshambuliaji toka Haiti Saint wakiwa wamefunga magoli mawili.


Huku Kipre Tcheche, Khamis Mcha na Kipre Bolue kila mmoja akifunga goli moja na kuifanya azam fc kuziona nyavu za wapinzani mara 10, huku nyavu zao zikichunguliwa mara 3.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.