Monday, August 18, 2014

JEMEDARI: EL MERREIKH NI KIPIMO TOSHA

Posted By: Unknown - 8:58 PM

Share

& Comment


http://m.habarileo.co.tz/images/resized/images/jemedari-said_300_147.jpg

MABINGWA wa soka wa Tanzania Bara, Azam FC imesema kucheza na El Merreikh ya Sudan katika robo fainali ya Kombe la Kagame, ni kipimo kizuri kwao.

Azam FC imeingia robo fainali juzi baada ya kuibamiza Atlabara ya Sudan Kusini kwa mabao 4-1 katika mechi ya mwisho ya makundi.

Timu hiyo ya Chamazi imeshika nafasi ya pili katika Kundi A kwa kuwa na pointi nane, mbili nyuma ya Rayon Sport inayoongoza kundi. Sasa itapambana na El Merreikh keshokutwa, na Meneja wa Azam FC, Jemedari Said anasema hicho ni kipimo sahihi kwao.

“Nilikueleza wakati tunakuja huku, kwamba tunakuja kushindana na kutwaa ubingwa. Sasa unapotaka kutwaa ubingwa, ni lazima ufanye kazi ngumu na sisi tunajua hii ni kazi ngumu. “Lakini hiki ni kipimo sahihi kwetu. El Merreikh ni moja ya timu zinazoheshimika kisoka katika ukanda huu, na yenye historia nzuri. Kwetu ni kipimo sahihi pia kwa maandalizi ya msimu ujao,” alisema Said kwa simu akiwa Kigali.

Alisema wataingia uwanjani wakiwa na nia moja ya kuendeleza wimbi la ushindi na kurejea na kombe katika michuano hiyo wanayoshiriki baada ya Yanga kufukuzwa kutokana na kupeleka majina ya wachezaji chipukizi.

Akizungumzia kuongoza kwao kwa kufunga mabao mengi wakiwa na mabao 10 hadi sasa, alisema hiyo ni muhimu kwani inawasaidia hasa katika michuano yenye ushindani kama hiyo.

“Hii ni silaha kwetu, tunaamini kuwa safu yetu ya ushambuliaji inafanya kazi yake,” alisema meneja huyo ambaye mshambuliaji wao, John Bocco anaongoza kwa kuwa na mabao matatu.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.