Azam FC hii leo wametinga robo fainali ya michuano ya kombe la Kagame kwa kishindo baada ya kuwachapa goli 4-1 Adama City ya Ethipia na kufikisha magoli 10 ya kufunga wakiwa wamejikusanyia pointi 8 katika michezo minne iliyoshuka dimbani.
Azam FC ilianza kuandika goli lake la kwanza katika dakika ya 22 kupitia kwa John Bocco akiunga krosi ya Khamisi Mcha.
Katika dakika ya 39 Adama City walisawazisha goli hilo kupia kwa Desaleny Debesh na kupelekea mchezo kwenda mapumziko kwa sare ya goli 1-1.
Kipindi cha pili kilianza kwa Adama City kusaka nafasi ya kujiongezea goli huku na Azam wakitafuta namna ya kupata goli la pili na la ushindi.
Katika dakika ya 51 Gadiel Michael ilimbidi aende benchi baada ya kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Said Morad na kupelekea Erasto Nyoni ambaye alikuwa mchezaji bora wa mchezo kwa mujibu wa Supersport kuhamia upande wa kushoto, huku upande wake ukichukuliwa na David Mwantika.
Mabadiliko hayo yaliongeza kasi ya ushambuliaji wa Azam FC kupitia upande wa kushoto ambao John Bocco na Nyoni ndio ulikuwa upande wao na mnamo dakika ya 55 mgusiano baina ya John Bocco na Erasto Nyoni uliza goli la paili kufuatia Didier Kavumbagu kuunga krosi ya Erasto Nyoni na kuiandikia Azam goli la pili.
Dakika tano mbele upande huo huo wa kushoto ulizalisha goli la tatu kupitia kwa Khamisi Mcha aliyeumalizia mpira uliotemwa na kipa wa Adama City na kuifanya Azam FC kuwa mbele kwa goli 3-1.
Erasto Nyoni kwa mara nyingine alihusika katika goli la nne lililofungwa na KIpre Hermani Tcheche akitumia vyema krosi ya Erasto nyoni na kupelekea mchezo kumalizika kwa ushindi wa goli 4-1.
Erasto Nyoni leo alicheza kwa mara ya kwanza toka mashindano yaanze akichukuwa nafasi ya Shomari Kapombe ambae ni majeruhi na kutumia vyema nafasi hiyo.
katika mchezo wa leo Azam FC walikuwa wanauwezo wa kufunga hata goli 7 kama Gardiel Michael angetumia vyema mipira aliyokuwa anatanguliziwa ambapo katika mipira minne aliyo tanguliziwa aliye utendea haki ni mmoja ambao Khamisi Mcha alipaisha akiunga krosi ya Gardiel Michael.
Azam FC Leo: Mwadini Ally, Erasto Nyoni, Gardile Michael/Said Morad, David Mwantika, Agrey Morice, Kipre Bolue, Salum Aboubakari/ Mudathir Yahya, Khamis Mcha/Farid Mussa, John Bocco, Didier Kavumbagu na Kipre Thceche
0 Maoni:
Post a Comment