Wednesday, August 13, 2014

KAVUMBAGU AANZA KUREJESHA FADHILA

Posted By: Unknown - 5:58 AM

Share

& Comment

Mshambuliaji wa kkimataifa wa Burundi Didier Kavumbagu jana aliokoa jaazi la Azam FC baada ya kuisawazishia Azam FC kwa kichwa akiunga krosi ya Kipre Tcheche na kupelekea mchezo kumalizika kwa sare ya kufungana goli 2-2.

Mchezo huo uliochezwa katika Uwanja wa Stade de Kigali, Nyamirambo Kavumbagu na Khamisi Mcha walianzia benchi huku nahodha John Bocco akikoseana kabisa katika mchezo huo,

Kavumbagu aliisawazishia Azam FC katika dakika ya 86 baada ya KIpre Tcheche kupokea pasi muruwa kutoka kwa Salum Aboubakari na Tcheche akapiga krosi iliyo mkutana Kavumbagu na kudumbukiza mpira kwenye nyavu.
Mkombozi; Didier Kavumbangu ameifungia bao la kusawazisha Azam FC leo Kigali

Azam ilikwenda kupumzika ikiwa inaongoza kwa bao 1-0 lililofungwa na kiungo Kipre Michael Balou kwa shuti la mpira wa adhabu kutoka umbali wa mita 20, baada ya pacha wake, Kipre Herman Tchetche kuangushwa.

Atlabara ilirudi vizuri kipindi cha pili na kufanikiwa kusawazisha bao dakika ya 48, mfungaji Nahodha wake, Thomas Batista kabla ya kufunga la pili dakika ya 60 mfungaji Bony Martin. 

Atlabara ilipata pigo dakika ya 89 baada ya Nahodha wake, Batista kutolewa nje kwa kadi nyekundu.
Shomary Kapombe akiruka kwenda chini baada ya kuchezewa rafu na beki wa Atlabara

Kwa matokeo hayo, Azam inafikisha pointi tano baada ya mechi tatu na kujihakikishia nafasi ya kwenda Robo Fainali ya michuano hiyo, wakati Atlabara inafikisha pointi mbili baada ya mechi mbili.

Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Aishi Manula, Gardiel Michael, Shomary Kapombe, Said Mourad, Aggrey Morris, Kipre Balou, Himid Mao, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Gaudence Mwaikimba/Didier Kavumbangu dk63, Leonel Saint Preux /Khamis Mcha dk63 na Kipre Tchetche. 

Atlabara; Jacko Mpenzi, Thomas Batista, Hamza Olema, Hatit Monydeng, Ibrahim Sebit, Kharim Mutawakil, Frando Justin Wani, Joseph Aquer, Dak Kujbor/Khamis Leon dk56 na Bony Martin.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.