Jaja leo alipata nafasi mbili nazo alizitumia vizuri kwa kuiandikia Yanga magoli mawili na kuifanya Yanga kuibuka na ushindi huo wa goli 3-0.
Katika mchezo huo wa leo wa ngao ya jamii uliochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam ulishuhudia timu zote mbili zikienda mapumziko wakiwa nguvu sawa.
Kipindi cha pili kilianza kwa Yanga kufanya mabadiliko ya kumtoa Nizar Khalfani na kumuingiza Saimon Msuva ambapo ilichukuwa dakika 10 tu kutengeneza goli la kwanza kwa Jaja katika mchezo wa leo,
Katika dakika ya 55 Haruna Niyonzima alimtangulizi Saimon Msuva na bila ajizi Msuva akamtolea pande Jaja na kuandika goli la kwanza kwa yanga.
Goli hilo liliwapoteza Azam FC na kupelekea kuruhusu goli la pili katika dakika ya 66 baada ya Jaja kukutana na kipa Mwadini Ally na kumtungua kirahisi.
Magoli hayo yalipelekea kocha Omega kumpumzisha Himid Mao na Leonal na nafasi zao kujazwa na Khamisi Mcha na Kelfin Friday.
Wakati mchezo unakimbilia mwishoni Yanga waliandika goli la 3 kupitia kwa Saimon Msuva akipokea mpira mrefu toka katika beki zake za Yanga na kufunga goli safi na kuipa Yanga Ngao ya Jamii.
Hii ni mara ya kwanza kwa kocha Omeg kuiongoza Azam FC ikipoteza mchezo kwa timu ya Tanzania huku na Azam wakifungwa kwa mara ya kwanza wakiwa wamevaa jzi zao za blue nyeusi (dark blue).
0 Maoni:
Post a Comment