Saturday, September 27, 2014

KAVUMBAGU AENDELEZA YAKE CHAMANZI, AZAM IKIUWA 2-0

Posted By: kj - 7:08 PM

Share

& Comment

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgn0ujj9awVFLvjFKzwWtNYHTsrFAugGigzcFtEJW14UsVfB_lDcXh_sMD0GfTuZXq_roQyMY5xWWRyEG649NsLPHAJ7beGn2iO91E846tzljaaN6RWoaLPIvY9As63vSBBL2NvwSfC9rk/s1600/KAVU+GOAL.jpg
Mshambuliaji wa Burundi Didier Kavumbagu ameendeleza wimbi la kuvumania nyavu baada ya leo kufunga magoli mawili na kufikisha magoli 4 katika mechi mbili alizoichezea azam fc katika ligi kuu ya vodacom.

Azam fc hii leo iliwalazimu kungoja mpaka dakika 40 ndio wafungua kurasa ya magoli ambapo Kavumbagu alimaliza mpira uliotemwa na kipa wa Ruvu shooting uliotokana na shuti la Kipre Tcheche.

Katika mchezo wa leo Azam fc na Ruvu shooting walikuwa wanashambuliana kwa awamu huku Azam FC wakifika mara nyingi kwenye goli la Ruvu shooting.

Katika kipindi cha pili azam fc walionekana kuwa tishio kulinganisha na kipindi cha kwanza na endapo washambuliaji wa azam fc wangekuwa makini wangefunga hata magoli hata manne.

Katika dakika ya 50 Kavumbagu aliifungia azam fc goli la pili, na kupelekea mchezo kumalizika kwa azam kuibuka na ushindi wa goli 2-0.

Kwa matokeo ya leo Azam FC wanaongoza ligi kwa kuwa na point 6, huku Kavumbagu akiongoza katika ufungaji wa magoli akiwa na magoli manne akuvuatiwa na Ami Ally na Ally Shomari wote kutoka Mtibwa Sugara na wote wakiwa na magoli mawili.

Jeshi la Azam Leo: Aishi Manula, Shomari Kapombe/Erasto Nyoni, Gardiel Michael, David Mwantika/Said Morad, Agrey Morice, Mudathir Yahya, Himid Mao/Farid Mussa, Kipre Bolue, Didier Kavumbagu, Salum Aboubakari, Kipre Tcheche .

KWA MATOKEO, MSIMAMO WA LIGI, NA RATIBA TEMBELEA www.amsuni.host56.com

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.