Monday, November 24, 2014

KIEMBA AIBUKA KWENYE MAZOEZI YA AZAM FC

Posted By: kj - 12:22 PM

Share

& Comment

Kiungo wa simba SC Amri Kiemba hii leo ameibuka katika mazoezi ya Azam FC yaliyo anza hii leo kwa ajili ya muendelezo wa ligi kuu ya vodacom itakayo endelea hapo desemba 26 mwaka huu.

Kiemba ambaye amekuwa akivumishwa kujiunga na Azam FC toka klabu yake ya Simba SC ilipo msimamisha kutokana na kucheza chini ya kiwango na hii leo ameonekana kwenye mazoezi ya Azam FC ikiwa ni siku ya kwanza ya mazoezi ya timu hiyo.

Mpaka sasa mtandao huu hauja pata taarifa ya kukamilika kwa dili la Kiemba kuamia Azam FC ila mtandao huu unafahamu kuwa Kiemba, Simba SC na Azam FC walikuwa kwenye maongezi ya kukamilisha dili hili
CHANZO: SPORT IN BONGO

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.