Saturday, December 20, 2014

AZAM FC WAPATA USHINDI WA KWANZA UGANDA, YAICHAPA VAIPER 3-1

Posted By: Unknown - 7:50 PM

Share

& Comment


Magoli mawili ya mshambuliaji wa Ivory coast anae kipiga Azam FC Kipre Herman Tcheche yalitosha kuipa Azam FC ushindi wa goli 3-1 dhidi ya vinara wa ligi kuu ya Uganda VIpers.

Katika mchezo hu wa kirafiki uliochezwa katika uwanja wa KCCA jijini Kampala Vipers FC walikuwa wa kwanza kupata goli katika dakika ya 17.

Katika dakika ya 30 Azam FC iliwabidi wafanye mabadiliko ya kumpeleka benchi Kipre Bolue baada ya kuumia na nafasi yake ikachukuliwa vyema na Amri Kiemba, mabadiliko hayo yalipelekea Salum Aboubakari kurejea nyuma na kumuacha Kiemba na Kavumbagu kuongoza safu ya ushambuliaji.
Mabadiliko hayo yalisababisha goli la kusawazisha la Azam FC kupitia kwa Kipre Tcheche akiunga krosi ya imid Mao.

Tcheche alirejea tena katika hesabu ya magoli kwa Azam FC baada ya kugongeana vyema na Mudathir Yahya na kukutana na kipa wa Viper na kudumbukiza mpira nyavuni.

Kipindi cha pili kilianza kwa Tcheche kwenda mapumziko na nafasi yake ikachukuliwa na Khamisi Mcha viali ambaye alifunga goli la tatu akiunga pasi ya kisigino ya Amri Kiemba na kuipa Azam FC ushindi wa goli 3-1.

AZam FC watacheza tena kesho dhidi ya KCCA kabla ya kuanza safari ya kurejea Tanzania kumalizi maandalizi ya kuendelea na duru la nane la ligi kuu ya vodacom.
 

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.