Sunday, December 21, 2014

AZAM WAHITIMISHA KWA KICHAPO TOKA KCCA WAKIWA PUNGUFU

Posted By: Unknown - 9:28 PM

Share

& Comment

Mabingwa wa Tanzania bara Azam FC hii leo wamemaliza ziara yao nchini Uganda kwakufungwa goli 2-0 na wenyeji wao KCCA, na kesho wanatarajia kuwasili nchini.

Azam FC katika walikuwa nchini Uganda kwa ziara ya michezo ya kirafiki ya kimataifa ambapo walifungua na SC Villa na kukubali kufungwa goli 3-2 kabla ya kufungwa goli n1-0 na URA na kufanikiwa kiuwafunga Viper goli 3-1.

Katika mchezo wa leo Azam FC waliwabidi wacheze dakika 60 wakiwa pungufu baada ya kiungo Himid Mao kuzawadiwa kadi nyekundu.
KCCA waliandika goli lao la kwanza katika dakika ya 17 kupitia kwaHerman Wasswa na dakika ya 72 kupitia kwa Brian Umonyi.

Kabla ya mchezo kuanza kocha wa Azam FC alisema kuwa michezo hiyo ya kirafiki aangalii sana matokeo bali wanaangalia nanma timu inavyocheza na kupelekea kunyenga timu ya ushindani hapo.

Azam FC inataraji kucheza mchezo wao wanane wa ligi kuu ya vodacom dhidi ya yanga hapo desemba 28 katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.