Wednesday, December 10, 2014

AZAM FC WAWACHAPA MTIBWA SUGAR 3

Posted By: Unknown - 6:12 AM

Share

& Comment

Mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania bara Azam fc wamefanikiwa kuwa funga vinara wa ligi kuu ya Tanzania bara goli 3-1, mchezo wa kirafiki uliochezwa jana usiku.

Katika mchezo huo wa kirafiki uliochezwa katika uwanja wa azam complex, ikiwa ni mara ya kwanza kwa azam fc kucheza usiku katika uwanja huo, ulishuhudiwa na mashabiki wa wastani.

Azam fc ndio walikuwa wa mwanzo kupata goli, lililofungwa na Didier Kavumbagu, baada ya kutokea rapsha katika langu la mtibwa na mpira kumkuta Kavumbagu aliyekwamisha mpira nyavuni.

Goli la pili la azam fc lilifungwa na Aggrey Morice kwa fataki kali lililo mshinda mlinda lango wa mtibwa sugar. Aggrey alifunga goli hilo baada ya kuanzishiwa mpira wa adhapu na Aggrey kuunga kama ulivyo.

Goli la mtibwa sugar lilifungwa na Mussa Hassan Mgosi kwa mkwaju wa penati, huku goli la mwisho la azam fc lilifungwa na Khamis Mcha na kupelekea mchezo kumalizika kwa azam fc kuibuka na ushindi wa goli 3-1.

Azam fc wanataraji kwenda Uganda wakati wowote ule kwa ajili ya michezo mingine ya kirafiki.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.