![]() |
Uwanja wa Azam Complex, utakao tumika kwa mchezo kati ya Mtibwa na Azam kesho usiku |
Mchezo wa kesho utakaichezwa katika uwanja wa Azam complex utakuwa mchezo wa kwanza kwa Azam FC kucheza usiku katika uwanja huo na huenda ukatumika kama sehemu ya kujaribu taa zilizofungwa katika uwanja wa huo.
Mtibwa Sugar wataingia kwenye mchezo huo wa kirafiki wakiwa na kumbukumbu ya kuwafunga Simba SC goli 4-2 katika mchezo wa kirafiki uliochezwa katika uwanja huo unao milikiwa na Azam FC.
Baada ya mchezo huo Azam FC watanzaa maandalizi ya safri ya kuelekea Uganda kwa usafiri wa basi, ambapo watacheza michezo mitatu ya kirafiki nchini humo.
Apo awali Azam FC ilitakiwa kwenda Zambia kwa ajili ya michezo ya kirafiki, na kutokana na kutokuwa na ligi na timu za ligi kuu za nchini humo kuwaruhusu wachezaji wao kwenda mapumzikoni,Uongozi wa Azam FC wameamua kuamisha safari yao nchini Uganda ambapo bado ligi yao inaendelea.
Azam FC watacheza mchezo wao wa kwanza wa kirafiki desemba 13 mwaka huu.
0 Maoni:
Post a Comment