Tuesday, December 23, 2014

AZAM KUFUNGUA NA EL-MERREKH KLABU BINGWA AFRIKA

Posted By: Unknown - 6:07 AM

Share

& Comment

MABINGWA wa Tanzania, Azam FC watamenyana na El Merreikh ya Sudan katika hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani.

Kwa mujibu wa ratiba ya Raundi ya Awali iliyopangwa jana mjini Cairo, mechi za kwanza zitachezwa kati ya Februari 13 na 15 wakati marudiano yatakuwa Februari 27 na Machi 1 na Azam FC wataanzia nyumbani.

Wakifanikiwa kuwatoa Wasudan hao, Azam FC watamenyana na mshindi kati ya Lydia Ludic B.A ya Burundi na Kabuscorp do Palanca ya Angola.

Wakati huo huo, Azam fc walirejea jana salama wakitokea Uganda kwa shirika la ndege la fast jet na kuingi kambini moja kwa moja wakijiwinda na mchezo wa ligi kuu ya vodacom dhidi ya yanga december 28 mwaka huu.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.