Wednesday, December 3, 2014

OMOG KUAMUA HATMA YA MUIVORYCOAST MWINGINE

Posted By: Unknown - 9:27 AM

Share

& Comment

http://www.ippmedia.com/media/picture/large/azam-sept19-2014.jpg
KLABU ya Azam FC imeonekana kunogewa na wachezaji wa Ivory Coast na sasa ina mpango wa kumsajili Sanaly Bamba kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho chenye makazi yake Chamanzi.

Tayari Azam ina wachezaji watatu wa Ivory Coast ambao ni Pascal Wawa aliyekuwa akikipiga El Mereikh ya Jamhuri ya Sudan, Kipre Tchetche na Kipre Bolou. Mchezaji huyo tayari yupo nchini kwa takriban wiki mbili akifanya mazoezi. Alitokea Nigeria alipokuwa akicheza soka.

Akizungumza na gazeti hili jana Meneja wa Azam FC Jemedari Said alisema Bamba atasajiliwa iwapo Kocha Mkuu wa klabu hiyo Joseph Omong na msaidizi wake George Nsimbe ‘Best’ watakubali kiwango chake.

“Bado anaendelea na mazoezi na hadi kufika Jumamosi tunategemea kupewa taarifa ya benchi la ufundi kama wamerizika naye au kama hawajarizika naye ili tuchukue hatua nyingine,” alisema.
Alisema Nsimbe ndio kwanza ameanza kazi tangu juzi hivyo anahitaji kumwona mchezaji huyo kisha kuungana na Omong katika maamuzi ya pamoja.

Wakati Nsimbe anatua nchini hivi karibuni alisema Uganda kuna wachezaji wengi wazuri wenye vipaji hivyo atatumia nafasi yake kuwasajili kwenye timu hiyo iweze kufanya vizuri.

Klabu hiyo ya Azam FC ilionesha nia ya kumsajili mshambuliaji wa Mali Mohamed Traore aliyekuwa akikipiga katika klabu ya El Mereikh lakini mpaka sasa haijawa wazi kama watamsajili ama la.

Azam inasajili kujiimarisha kutetea taji lake la Ligi Kuu, haina mwenendo mbaya kwenye ligi kwani inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 13 sawa na Yanga iliyo nafasi ya pili. Kinara wa ligi hiyo ni Mtibwa Sugar ikikaa kileleni kwa pointi 15.

CHANZO: HABARI LEO

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.