KOCHA Mkuu wa klabu ya soka ya Azam FC, Joseph Omog, amesema wana kazi kubwa ya kufanya ili kuwatoa wapinzani wao El Merreikh ya Sudan katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Shirikisho la Soka Afrika (CAF), juzi lilipanga ratiba ya mashindano hayo ya ngazi ya klabu na kuipanga Azam kuanza na mabingwa hao wa Afrika Mashariki na Kati huku Yanga ikipangwa kuanza na BDF IX ya Botswana katika michuano ya Kombe la Shirikisho.
“Naiheshimu El Merreikh, ni moja ya timu kubwa na nzuri katika ukanda huu wa Afrika lakini nitahakikisha tunafanya kila tunaloweza ili tuweze kupambana nao na kuwatoa japo siyo kazi nyepesi,” alisema Omog.
Omog alisema kwa kutambua hilo atahakikisha wanafanya mazoezi ya nguvu na kuwapa wachezaji mbinu mbadala ili kufanikisha lengo lao la kuitoa timu hiyo na kufika mbali kwenye mashindano ya mwaka huu na siyo kutolewa mapema kama ilivyokuwa mwaka jana kwenye Kombe la Shirikisho.
“Najua mechi za ligi zitatusaidia, lakini pia nitahakikisha tunaongeza muda wa mazoezi ili tuweze kufanikisha lengo letu kwa sababu tumepanga kufika mbali mwaka huu na siyo kutolewa kwenye hatua ya awali kama ilivyokuwa mwaka jana,” alisema Omog.
Kocha huyo raia wa Cameroon, alizungumzia kambi yao ya siku 10 waliyoweka Uganda na kucheza mechi nne za kirafiki na kusema ilikuwa nzuri na yenye mafanikio makubwa licha ya kufungwa mechi tatu walizocheza huko.
“Tumeweza kujifundisha mambo mengi ambayo naamini yatatusaidia kwenye ligi pamoja na mashindano ya kimataifa tunayotarajia kucheza mwakani, lengo la kwenda Uganda lilikuwa ni kujua mapungufu yetu tunapocheza na timu za nje ya Tanzania nashukuru tumeyajua,” alisema Omog.
Azam ambao ni mabingwa watetezi wa taji la Ligi Kuu Tanzania Bara, Jumapili ya wiki hii inatarajia kupambana na Yanga ukiwa ni mchezo wa raundi ya nane wa Ligi Kuu utakaopigwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
CHANZO: HABARI LEO
Shirikisho la Soka Afrika (CAF), juzi lilipanga ratiba ya mashindano hayo ya ngazi ya klabu na kuipanga Azam kuanza na mabingwa hao wa Afrika Mashariki na Kati huku Yanga ikipangwa kuanza na BDF IX ya Botswana katika michuano ya Kombe la Shirikisho.
“Naiheshimu El Merreikh, ni moja ya timu kubwa na nzuri katika ukanda huu wa Afrika lakini nitahakikisha tunafanya kila tunaloweza ili tuweze kupambana nao na kuwatoa japo siyo kazi nyepesi,” alisema Omog.
Omog alisema kwa kutambua hilo atahakikisha wanafanya mazoezi ya nguvu na kuwapa wachezaji mbinu mbadala ili kufanikisha lengo lao la kuitoa timu hiyo na kufika mbali kwenye mashindano ya mwaka huu na siyo kutolewa mapema kama ilivyokuwa mwaka jana kwenye Kombe la Shirikisho.
Kocha huyo raia wa Cameroon, alizungumzia kambi yao ya siku 10 waliyoweka Uganda na kucheza mechi nne za kirafiki na kusema ilikuwa nzuri na yenye mafanikio makubwa licha ya kufungwa mechi tatu walizocheza huko.
“Tumeweza kujifundisha mambo mengi ambayo naamini yatatusaidia kwenye ligi pamoja na mashindano ya kimataifa tunayotarajia kucheza mwakani, lengo la kwenda Uganda lilikuwa ni kujua mapungufu yetu tunapocheza na timu za nje ya Tanzania nashukuru tumeyajua,” alisema Omog.
Azam ambao ni mabingwa watetezi wa taji la Ligi Kuu Tanzania Bara, Jumapili ya wiki hii inatarajia kupambana na Yanga ukiwa ni mchezo wa raundi ya nane wa Ligi Kuu utakaopigwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
CHANZO: HABARI LEO
0 Maoni:
Post a Comment