Mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania bara Azam fc wametoa sare na mabingwa watetezi wakombe la mapinduzi KCCA katika mchezo wa pili wa kundi B katika mashindano ya kombe la mapinduzi.
Katika mchezo huo ulioanza saa 11 jioni katika uwanja wa Amani kisiwani Unguja ulishuhudia Azam fc na KCCA wakimaliza mchezo kwa kufungana goli 2-2.
Azam fc walikuwa wa mwanzo kupata goli kupitia kwa John Bocco katika dakika ya 38 akiunga krosi ya Mganda Brian Majwega, na kupelekea Azam fc kwendamapumziko wakiwa mbele kwa goli 1-0.
Katika kipindi cha pili KCCA waliingia na kasi na kufanikiwa kusawazisha katika dakika ya 49, kupitia kwa William Waori ambapo aliachia shuti la umbali wa mita 22.
Dakika 6 baada ya goli hilo Azam fc waliongeza goli la pili kupitia kwa Salum Abubakar 'Sure Boy' aliyeunganisha kwa kichwa kona ya Majwega.
KCCA ilisawazisha bao hilo dakika ya 73 kupitia kwa Tom Masiko aliyepiga mpira wa adhabu uliotinga moja kwa moja nyavuni, baada ya yeye mwenyewe kuchezewa rafu na Erasto Nyoni.
Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Mwadini Ali, Shomary Kapombe, Erasto Nyoni, David Mwantika, Aggrey Morris, Mudathir Yahya, Himid Mao/Kelvin Friday dk75, Salum Abubakar, John Bocco/ Gaudence Mwaikimba dk89, Amri Kiemba/Waziri Salum dk39 na Brian Majwega.
Katika mchezo wa saa tisa wa kundi B kati ya KMKM na Mtende ulimalizaki kwa sare ya bila kufungana.
MSIMAMO KUNDI B
Azam fc 1 1
KCCA 1 1
KMKM 1 1
Mtende 1 1

0 Maoni:
Post a Comment