Saturday, January 3, 2015

MZEE WA RIKODI NDANI YA AZAM FC

Posted By: Unknown - 10:08 AM

Share

& Comment

Captain John Rafael Bocco amendelea kuandika historia ndani ya klabu yetu. Baada ya kufunga magoli mawili mjini Dodoma mwaka 2008 ambayo ndio yaliipandisha timu daraja na kucheza Ligi kuu, mwaka 2014 pale Jijini Mbeya alifunga goli lililoipa timu ubingwa wake wa kwanza wa ligi kuu dhidi ya Mbeya City.
Tarehe 28 Desemba 2014 alifunga goli dhidi ya Yanga uwanja wa Taifa ukiwa mpira wake wa kwanza kuugusa tangu aingie kiwanjani kuchukua nafasi ya Salum Abubakar. Goli hilo ndio lilikua la mwisho kufungwa na Azam FC kwa mwaka 2014!

Lakini pia jana alifunga goli la mwanzo la kimashindano kwa Azam FC kwa mwaka mpya wa 2015 huku beji ya unahodha ikivaliwa na yeye kwa mara ya kwanza mwaka huu!

Na nimfungaji bora wa azam fc wakati wote.

Ahsante sana Captain Bocco.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.