Thursday, February 19, 2015

AZAM FC WAPUNGUZWA KASI NA RUVU SHOOTING

Posted By: kj - 6:27 PM

Share

& Comment

http://www.azamfc.co.tz/sites/default/files/imagecache/slides/azam%20kikosi%20web_0.JPG
Mabingwa wa ligi kuu ya vodacom Azam FC hii leo wamepunguzwa kasi na Ruvu shooting baada ya kutoka sare ya bila kufungana katika mchezo wa ligi kuu ya vodacom uliochezwa katika uwanja wa Mabatini mkoani Pwani.
Katika mchezo huo ambao ulishuhudia timu zote zikishinda kuona nyavu za wapinzani wao, kitendo kilicho sababishwa na uimara wa goli kipa wakila pande ambapo walifanya kazi ya ziada katika kuihakikishia timu yake walu pointi moja.

Katika kipindi cha kwanza kama Kipre Herman Tcheche angekuwa makini basi angeipatia goli Azam FC kufuatia shuti lake kutoka nnje ya goli alipo baki na kipa.

Mchezo huo haukuwa na ufndi wa aina yoyote ile kutokana na ubovu wa eneo la kucheza kitendo kilichopelekea timu zote kutumia mipira mirefu, na kutengeneza nafasi chache ambazo zilikuwa zina ishia mikononi mwa magoli kipa.

Kwa matokeo hayo Azam FC wameteremka mpaka nafasi ya pili na kuwa nyuma kwa pointi mbili dhidi ya vinara yanga wenye pointi 28 azan fc wakiwa na pointi 26.

Azam FC watacheza tena mchezo wa ligi kuu ya vodacom dhidi ya Tanzania Prisons siku ya jumapili katika uwanja wa Azam complex.

Azam FC leo: Aishi Manula, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Said Morad, Pascal Wawa, Mudathir Yahya, Himid Mao, Salum Aboubakari, John Bocco, Franky Domayo\ Didier Kavumbagu, Kipre Tcheche/Kelvin Friday

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © 2025 CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.