Thursday, February 19, 2015

OMOG: TUTAFIKA MBALI

Posted By: kj - 9:49 AM

Share

& Comment


https://fbcdn-photos-f-a.akamaihd.net/hphotos-ak-xpf1/v/t1.0-0/10942505_913317738708583_7474104849745880762_n.jpg?efg=eyJpIjoiYiJ9&oh=3c0b95e40f484e7e4ad081d86f1ec062&oe=554874BE&__gda__=1431711700_72e9c37e4c79ac1cd487e0effb8a23ae

KOCHA wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Tanzania bara Azam, Joseph Omog, amesema atatumia uzoefu wake aliokuwa nao kwenye michuano ya kimataifa kuifikisha mbali timu hiyo.

Omog, raia wa Cameroon baada ya kukiongoza kikosi chake kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya El Merreikh ya Sudan alisema hakuna kinachoshindana kutokana na uimara wa kikosi alichokuwa nacho msimu huu.

“Nilijaribu msimu uliopita lakini nilikuwa na kikosi dhaifu ambacho nilikikuta na tulitolewa mapema na Ferroviário Beira ya Msumbiji lakini mwaka huu nimeirekebisha timu kwa asilimia kubwa kwa kusajili wachezaji wenye uzoefu ambao naamini tunaweza kufikia lengo letu,” alisema Omog.

Omog aliyewahi kuchukua ubingwa wa kombe la Shirikisho Afrika akiwa na kikosi cha AC Leopard ya Congo mwaka 2012, alisema kwa maandalizi waliyofanya anauhakika wataiondosha El Merreikh katika mchezo wa marudiano licha ya ubora wa timu hiyo kutoka Sudan.

“Tumejiandaa kwa muda mrefu na matokeo ya Jumapili ni uthibitisho wa kile ambacho tulikwenda kukifanya kwenye nchi za Uganda na DR Congo lengo letu mwaka huu ni kutwaa makombe mawili makubwa la kwanza ni ubingwa wa Tanzania bara na pili ni Ligi ya Mabingwa Afrika,” alisema Omog.

Kocha huyo alisema pamoja na michuano hiyo kuwa na ugumu mkubwa lakini anahakika watafanya vizuri na Azam itajulikana Afrika nzima kama zilivyo timu kubwa kama TP Mazembe ya DR Congo, Zamalek na Al Ahly za Msri.

Azam inayoundwa na nyota watano wa kimataifa kutoka nchi za Ivory Coast, Burundi na Nigeria inaongoza Ligi Kuu Tanzania bara ikiwa na pointi 25 na pia imejiwekea mazingira mazuri ya kusonga mbele katika michuano ya Ligi ya Mabingwa kwa kuifunga El Merreikh mabao 2-0 hivyo kuhitaji sare katika mchezo wa marudiano ili iweze kusonga mbele. 


CHANZO: HABARI LEO

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © 2025 CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.