Sunday, February 22, 2015

AZAM WAVUNA 2 TOKA KWA PRISONS TENA

Posted By: Unknown - 10:32 PM

Share

& Comment

Mabingwa wa ligi kuu ya vodacom Azam fc wamepata pointi 2 katika michezo miwili dhidi ya Tanzania Prisons msimu huu kama ilivyokuwa kwa msimu uliopita.

Azam fc usiku wa leo wametoka sare ya bila kufungana na Tanzania Prinsons ikiwa ni kama mchezo wa oktoba 4 mwaka jana uliochezwa katika uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya.

Katika mchezo wa leo kipa wa Prisons alifanya kazi ya ziada kuhakikisha azam fc hawapati goli lolote lile, kwa kuokoa hatari zote zilizokuwa zinaelekezwa kwake, katika mchezo ambao Prisons muda mrefu walikuwa nyuma wakizuia.

Kwa kipindi chote cha mchezo Prisons walikuwa katika eneo lao na kuwaacha azam fc wachezee mpira wanavyotaka, huku wakiwanyima mianya ya kutengeneza nafasi ya kupata goli.

Kwa matokeo ya leo Azam fc wanabakia katika nafasi yao ya 2 wakiwa na point 27 wakati vinara yanga wakiwa na pointi 31 na kagera sugar wanaoshika nafasi ya 3 akiwa na pointi 24.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.