Monday, February 23, 2015

AZAM KWENDA SUDAN KESHO

Posted By: Unknown - 10:06 PM

Share

& Comment

Kikosi cha mabingwa wa Tanzania bara Azam fc kinataraji kuondoka nchini hapo kesho usiku kwa kutumia shirika la ndege ya Kenya, kuelekea Sudan kwa ajili ya mchezo wa marejeano wa klabu bingwa Afrika utakao chezwa siku ya jumamosi usiku.

Kwa mujibu wa kauli ya meneja wa Azam FC Jemedari Said alipokuwa anahojiwa na kituo kimoja cha redio nchini amesema kuwa msafara huo utakuwa na wachezaji 21 pamoja na viongozi 8 wa benchi la ufundi.

Azam fc wanahitaji sare ya aina yoyote ile ili iingie katika hatua ya kwanza ya michuano hiyo, ikiwa ni baada ya kuibuka na ushindi wa goli 2-0 katika uwanja wa azam complexs.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.