Saturday, February 28, 2015

AZAM WAPIGWA STOP CAF MWAKA HUU

Posted By: Unknown - 10:41 PM

Share

& Comment

https://scontent-lhr.xx.fbcdn.net/hphotos-xpa1/v/t1.0-0/10919016_919274534779570_5319681622089365783_n.jpg?efg=eyJpIjoiYiJ9&oh=afd8398ee67d70dee5225d62e6e8260e&oe=5595170D
Mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania Bara Azam Fc imetolewa na El-merekh katika klabu bingwa Afrika baada ya leo kukubali kichapo cha goli 3-0 katika uwanja wa Al-merekh nchini Sudan.

Azam FC waliingia katika mchezo wa leo wakiwa na akiba ya magoli 2-0 waliyopata katika mchezo wa kwanza uliochezwa katika uwanja wa Azam complex, wameshindwa kuulinda na hatimaye kujikuta wakiondolewa kwajumla ya goli 3-2.

Katika mchezo wa loe Azam Fc walianza taratibu huku wapinzani wao El-merekh wakiuwanza kwa kasi na kufanikiwa kupata goli katika dakika ya 19 kupitia kwa Mohammed Traore

Kuingia kwa goli hilo kuliwashtua Azam FC na kuanza kupeleka mashambulizi langoni mwa El merekh bila mafanikio na kupelekea mchezo kwenda mapumziko El-merekh wakiwa mbele kwa goli 1-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi, kwa kila upande kusaka goli, ila kadri ya muda ulivyosogea Azam FC walikuwa wanazidi kurudi nyuma kuzia wasiruhusu goli lolote lilile.

Wakati baadhi ya mashabiki wakianza kutoka Ahmed Ally Abdallah aliiandikia goli la pili El-merekh katika dakika ya 85 na kuibua shangwe za mashabiki wa El-merekh ambao walikwisha kata tamaa.

Kuingia kwa goli hilo kulipelekea Azam FC kwenda mbele kusaka goli huku El-merekh nao wakisaka goli la kuwavisha kwenda hatua inayofuata.

Alikuwa mtokea benchi aliyeingiaa kuchukuwa nafasi ya Mohamed Raore, Allan Wanga kuiandika El-merekh goli la 3 na la ushindi katika dakika ya 89.

Kwa matokeo hayo El-merekh wameitoa Azam FC kwa jumla ya magoli 3-2, kutokana na Azam FC kushinda goli 2-0 katika mchezo wa awali uliochezwa katika uwanja wa Azam complex. 

Azam FC leo: Aishi Manula, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Aggrey Morice, Pascal Wawa, Kipre Bolue/Franky Domayo, Himidi Mao, Salum Aboubakari, Didier Kavumbagu, Kipre Tcheche/Said Morad, Brian Majegwa/John Bocco.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.