Saturday, February 7, 2015

POLISI YAIPUNGUZA KASI AZAM FC

Posted By: kj - 6:44 PM

Share

& Comment


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEih4c5Z9AtDb1r0wRDP7eVLVCqbTlMIgjgnrUS4WxC1KzusgMzDbX4ofPxLLhESppn-ONFDxrmagSeshUW7kdxUOSCPVTonXq3Z4HZMhPbYsP519QJOJMBRSIvyx3hyphenhyphenLG0y2sGQLtcfyfhV/s1600/10847549_808297752551709_8272495318791573431_o-790072.jpg
Mabingwa wa ligi kuu ya vodacom Azam FC leo wamepunguzwaq kasi na Polisi MOrogoro baada ya kwenda sar ya goli 2-2 katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.

Katika mchezo huo uliotawaliwa na maamuzi ya utata Azam FC walikuwa wa mwanzo kupata goli kupitia kwa Kipre Tcheche baada ya shuti lake kumgonga beki wa Polisi Morogoro na mira kutinga nyavuni katika dakika ya 12.

Kuingia kwa goli hilo liliongeza kasi ya mchezo ambapo Polisi Morogro walikuwa wanasaka goli la kusawazisha wakati Aam Fc wakisaka goli la kuongoza.

Polisi Morogoro ambao leo walikuwa vizuri katika eneo la katikati ya uwanja walisawawzisha goli kupitia kwa Edward Christopher goli lillo leta utata na kupelekea wachezaji wa Azam FC kumzonga mwamuzi wa mchezo.

Hadi mapumziko Azam FC na Polisi Morogoro walikuwa wamefungana goli 1-1, na kupelekea kipindi cha pili kuanza kwa kushambuliana kwa kushtukiza, wakati Polisi Morogoro wakitawala eneo la kati.

Azam FC waliandika goli la pili katika dakika ya 65 kupitia kwa Kipre Bolue, aliyepiga mpira wa faulo ambao ulimgonga Selemani Kasim Selembe na Mpira kutinga nyavuni.

Selembe Aliisawazishia Polisi Morogoro katika dakika ya 80 akiunga kwa kichwa mpira wa faulo na kupelekea mchezo kumalizika kwa sare ya goli 2-2.

Azam FC wamerejea kileleni kwa muda baada ya kufikisha point 22 sawa na yanga ila wakiwazidi yanga goli moja katika tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa.

Azam FC leo: Aishi Salum, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Pascal Wawa, Said Morad, Kipre Bolue, Salum Aboubakari, Franky Domayo/Mudathi Yahya, Didier Kavumbagu, Kipre Tcheche/Kelvin Friday, Brian Majegwa/John Bocco.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.