Tuesday, April 14, 2015

AZAM FC KUIKABILI MGAMBO KESHO, SURE BOY KUREJEA

Posted By: Unknown - 3:10 PM

Share

& Comment


Kiungo mchezeshaji wa Azam FC Salum Aboubakari anatarajiwa kuwemo kwenye kikosi kitakacho wakabili Mgambo shooting hapo kesho katika muendelezo wa michezo wa ligi kuu ya vodacom.

Azam FC kesho watakuwa wageni wa Mgambo shooting katika uwanja wa CCM Mkwakwani, mchezo uliotakiwa uchezwa mwanzoni mwa mwaka huu.

Azam FC inaingia katika mchezo huo bila ya nahodha wake John Bocco, sambamba na Kipre Tcheche na Agrey Morice walio majeruh, na vilevile wanataraji kukosa huduma ya beki Davud Mwantika aliyerejea kwao kumuuguza babaake.

Pamoja na kuwakosa nyota hao, mchezo wa kesho ni muhimu kwa upande wa Azam FC katika harakati ya kutaka kutetea ubingwa wake wa ligi kuu ya Tanzania bara.

Kurejea kwa Sure Boy baada ya kukosekana katika michezo 4 ya ligi kuu ya vodacom kunaongeza uimara katika safu ya kiungo.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.