Wednesday, April 15, 2015

KHAMISI MCHA AFIWA NA BABA AKE

Posted By: Unknown - 11:17 AM

Share

& Comment



Baba mzazi wa mchezaji wa timu ya Taifa na Azam FC Khamis Mcha 'Viali', Mzee Mcha Khamisi amefariki hapo jana usiku.

Mzee Mcha Khamis amepatwa na umauti jijini Dar es salaam ambako alikuja kupata matibabu.
 
Mzee Mcha Khamis, baba wa Khamis Mcha (pichani), katika uhai wake amepata kuitumikia timu ya KMKM na Miembeni pamoja na timu ya taifa ya Zanzibar (Zanzibar heroes).

 Mtandao wa Aboodmsuni Network inampa pole Khamisi Mcha kwa kutokwa na mzazi wake, pamoja na familia yake na wawe na subra katika kipindi hiki kigumu. Innalillah wa innaillaih rajiun!

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.