Wednesday, April 15, 2015

SARE ZENDELEA KUIANDAMA AZAM FC, NAFSI VINYU YA KUTETEA UBINGWA

Posted By: kj - 6:24 PM

Share

& Comment

Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya vodacom, Azam FC wameendeleza wimbi lao la sare baada ya leo kwenda sare ya 3 mfululizo katika michezo ya lgi kuu ya vodacom.
Azam FC leo walikuwa wageni wa Mgambo shooting ambapo dakika 90 zilmalizika kwa sare ya bila kufungana, huku Azam Fc wakimaliza wakiwa pungufu.

Katika dakika 70 za mwanzo za mchezo, timu zote zilikuwa zinashambuliana kwa zamu, na mchezo kuwa sawa kwa pande zote mbili.

Hali ilikuwa ngumu kwa Azam FC mara baada ya kiungo Himid Mao Mkame kuzawadiwa kadi nyekundu kwa kumchezea vibaya kiungo Ful Zul Maganga katika dakika ya 70.

Katika dakika ya 20 za mwisho wa mchezo Mgombo shooting wametengeneza nafasi mbili zawazi, ambazo zingeweza kuipatia ushindi wa goli 2-0 katika mchezo wa leo.

Kwa matokeo hayo Azam Fc ni kama wamejioa katika mbio za ubingwa baada ya kuachwa na yanga kwa jumla ya pointi 7 huku kukisalia michezo mitano kwa kila mmoja.

Azam FC leo: Aishi Manula, Shomari Kapombe, Gardiel Michael, Erasto Nyoni, Pascal Wawa, Kipre Bolue/ Franky Domayo, Himid Mao, Salum Aboubakari/Mudathir Yahya, Gaudency Mwaikimba, Dider Kavumbagu/Amri Kiemba na Brian Majegwa.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.