Mshambuliaji mpya wa Azam,Allan Wanga amesema ametua kwenye timu hiyo kwa ajili ya kuipa taji la pili la ubingwa wa Tanzania Bara.
Wanga ambaye wiki hii alirejea kwao Nairobi kufuatia kifo cha Mama yake Mzazi amesema anajua vizuri ushindani wa Ligi ya Tanzania na haoni sababu ya kushindwa kutimiza malengo yake ya kuipa ubingwa timu hiyo aliyojiunga nayo akitokea El Merreikh ya Sudan.
“Nipo hapa kwa wiki tatu sasa nimefanya mazoezi ya kutosha nimezoeana vizuri na wachezaji wenzangu kazi yangu kwa sasa ni moja kuipa ubingwa Azam kama ambavyo nimeuahidi uongozi,”amesema Wanga ambaye ni mchezaji wa Harambee Stars na FC Leopard ya Kenya.
Wanga ametua Azam ambao ndio mabingwa wapya wa Kombe la Kagame anatarajiwa kupewa majumu ya kuongoza mashambulizi ya timu hiyo sambamba na nahodha John Bocco katika michuano ya Ligi ya Vodacom inayotarajia kuanza Septemba12 ,2015.
CHANZO: KANDANDA.CO.TZ
0 Maoni:
Post a Comment