Nahodha na mshambuliaji wa Azam FC John Bocco akikimbia kushangilia baada ya kuifungia timu yake goli la kwanza kwenye mchezo wa fainali ya kombe la Kagame dhidi ya Gor Mahia ya Kenya |
Bocco: Kwanza namshukuru Mungu na timu yote kwa ujumla tunamshukuru Mungu, kwasababu safari ya Kagame ilikuwa ndefu halafu ngumu. Tunamshukuru Mungu tumeweza kushinda tumekuwa mabingwa, tumemaliza salama pia ninachofurahi zaidi nimeona timu yetu ilivyokua zaidi kwasababu msimu ule tumefika fainali na Yanga timu yetu ilikuwa bado changa kwenye mashindano ya kimataifa nachomshuru Mungu sasahivi tumeonesha ukomavu kuwa tupo zaidi kimataifa na tutafanya vizuri.
Swali: Sasahivi mashindano ya Kagame yamemalizika na nyinyi mmetwaa ubingwa mnajiandaa kwa ligi na michuano ya kimataifa unawaambia nini mashabiki wa Azam?
Bocco: Ninacho waambia waendelee kutuamini, waendelee kutusapoti kama walivyotusapoti, waamini Azam ni timu kubwa sasa sio timu ndogo na inacheza kwa nguvu na kujituma ili iweze kufanya vizuri na kubadilisha mpira wa Tanzania kwahiyo wawe na matumaini makubwa kwa Azam.
Swali: Watanzania waliojitokeza uwanjani walikuwa wanaipa sapoti Azam tofauti na mechi zilizopita kwamba kulikuwa na mgawanyiko unakuta mashabiki wanashangilia timu tofauti, wewe hili unalizungumziaje?
Bocco: Ni kitu cha faraja sio kwa Azam tu, ni faraja kwa nchi nzima kwasababu kama mashabiki wa timu nyingine wanaweza kuja kuisapoti timu nyingine kwa hatua kama hii ni kitu kizuri sana kinatia faraja, kwahiyo mimi nafurahi waendelee kama hivi wasiweke makundi tukifika kwenye mechi za kimataifa kama hivi. Walete upinzani wao wanapokutana wao kwa wao lakini ikifikia kitu cha kitaifa waweke uzalendo mbele waweze kulisapoti taifa kwasababu leo Azam ilikuwa inawakilisha taifa kwa ujumla. Kwahiyo kama hivi ni kitu kizuri sana kwa nchi pia kitasaidia hata kupandisha mpira weu wa Tanzania.
Hapa chini kuna sauti ya John Bocco, bofya ili kumikiliza….
0 Maoni:
Post a Comment