Thursday, August 27, 2015

AZAM FC KUELEKEA MTWARA KESHO, KUWAKABILI NDANDA JUMAMOSI

Posted By: kj - 8:10 PM

Share

& Comment

Kikosi cha mabingwa wa Afrika mashariki na kati Azam FC kesho watasafiri kuelekea Mtwara kwa ajili ya mchezo wa kirafiki utakao chezwa siku ya jumamosi dhidi ya Ndanda FC ya Mtwara.

Mchezo huo wa kirafikia maalum kwa ajili ya kuazimisha siku ya Ndanda FC utachezwa katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara.

Afisa habari wa Azam FC Japhari Iddi Maganga amesema kuwa kikosi hiko kinacho kosa nyota wake takribina 11 waliopo kwenye timu zao za Taifa kitaelekea Mtwara kesho na kurejea jijini Dar es saalm siku ya jumapili baada ya kucheza na Ndanda FC katika uwanja wa Nangwanda sijaona.

Maganga ameongeza kuwa baada ya kurejea wanataraji kucheza mchezo wa mwisho wa kirafiki dhidi ya JKT Ruvu katika uwanja wa Azam Complex kabla ya kuanza mikimiki ya ligi kuu ya vodacom.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.