Wednesday, August 26, 2015

AZAM FC WATOA SARE YA MWADUI, WAKIRUHUSU GOLI KATIKA NYAVU ZAO

Posted By: kj - 9:18 PM

Share

& Comment

Mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati Azam FC wametoa sare ya goli 1-1 na Mwadui FC katika mchezo wa kirafiki uliochezwa leo katika uwanja wa Azam complex, na rikodi yao ya kucheza michezo 13 bila ya kuruhusu goli ikivunjwa.

Katika kipindi cha kwanza Azam FC waliutawala mchezo huku kiungo Ramadhan Singano akiwatengenezea nafasi ya kufunga Shabaani Iddi na Amme Ally waliyoshindwa kuzitumia.

Mwadui walitumia muda mwingi kuzuia huku wakipeleka mashambulizi ya kushtukiza, ambapo Paul Nonga na Jerry Tegete walipoteza nafasi kwa nyakati tofauti na kupelekea kipindi cha kwanza kumalizika kwa sare ya bila kufungana.

Katika kipindi cha pili Azam FC walianza kwa kufanya mabadiliko kwa kumpumzisha Shabaani Iddi na nafasi yake kuchukuliwa na Kipre Tcheche mabadiliko yaliyoendeleza kasi ya Azam FC kuliandama lango la Mwadui FC.

Alikuwa Ramadhan Singano aliyeiandikia Azam FC goli pekee katika mchezo wa leo baada ya kupiga mpira uliotnga moja kwa moja langoni akitokea pembeni upande wa kulia katika dakika ya 47 ya mchezo.

Kuingia kwa goli hilo kulipekea Mwadui FC kufanya mabadiliko kadhaa ambayo yaliwasaidia kurejea mchezoni na katika dakika ya 70 kupitia kwa Abdalla Kigodeko walifanikiwa kusawazisha goli hilo na kupelekea mchezo kumalizika kwa sare ya ya goli 1-1.

Mara ya mwisho kwa Azam FC kuruhusu goli katika nyavu zake ilikuwa dhidi ya Friends Ranger ambapo Azam FC walishinda goli 4-2, mchezo uliochezwa katika uwanja wa Azam Complex, baada ya mchezo huo wamecheza michezo 13 ikiwemo ya Kagame Cup na ya kirafiki bila kuruhusu nyavu zao kuguswa.

Azam FC leo: Mwadini Ally, Erasto Nyoni, Aggrey Morrice, Pascal Wawa, David Mwantika/Abdallah Kheri, Gardiel Michael, Salum Abubakari, Briyson Raphael/Prosper Prosper, Amme Ally/Kelvin Friday, Shaban Iddi/Kipre Tcheche, Ramadhan Singano/Khamis Mcha.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.