Katika mchezo wa leo JKU waliuwanza mchezo kwa kasi na ndani ya dakika 3 walikuwa wamefika goli mwa Azam mara tatu na kufanya majaribio ya kumjaribu kipa Mwadini Ally ambaye alifanya kazi yake vyema.
Kadri ya dakika zilivyokuwa zinasogea kasi ya JKU ilikuwa inapunguwa na kuwapa nafasi Azam FC kuingia mchezoni taratibu na kutengeneza nafasi chache katika kipindi hicho cha kwanza ambapo timu zote zilikwenda mapumziko wakiwa sare ya bila kufungana.
Kipindi cha pili kilianza kwa kuingia Mudathir Yahya na Amme Ally kuchukuwa nafasi ya Jean Mugereneza na Franky Domayo, mabadiliko yaliyo ongeza kasi ya Azam FC na kuanza kusakata soka la uahikika zaidi.
Alikuwa nahodha John Raphael Bocco katika dakika 57 aliiandikia Azam FC goli la kwanza katika mchezo huo akiunga mpira wa Mudathir Yahya.
Katika dakika ya 86 Salum Abubakari 'Sure Boy' aliifungia Azam FC goli la pili akipokea pasi kutoka kwa Ame Ally Zungu na kupelekea mchezo kumalizika kwa Azam FC kuibuka na ushindi wa goli 2-0.
Azam FC leo: Mwadini Ali-1, Shomari Kapombe/Khamis Mcha, Shah Farid Musa/Ramadhan Singano, Agrey Morris/Said Morad, Pascal Wawa, Erasto Nyoni/David Mwantika, Jean Mugiraneza/Mudathir Yahya, Himid Mao, Franky Domayo/Amme Ally, John Bocco, Kipre Tchetche/Salum Abubakaria
0 Maoni:
Post a Comment