Kavumbagu na Farid Mussa Maliki wakishangilia goli la kwanza la AZam FC lililo fungwa na Kavumbagu |
Katika mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam Azam FC waliuwanza mchezo kwa kasi na katika dakika ya kwanza Azam FC walikuwa teyari wameshafika langoni mwa JKT Ruvu.
Katika dakika ya 4 Dider Kavumbagu akicheza mchezo wake wa kwanza msimu huu aliiandikia Azam FC goli la kuongoza akimaliza pasi ya Michael Bolue aliyekuwa anaanza kwa mara ya pili msimu huu.
Wakati JKT Ruvu wakiwa wamebutwaa na goli hilo la kwanza, JOhn Bocco aliandikia Azam FC goli la pili katika dakika ya 7 ya mchezo.
Baada ya Bocco kuandika goli la pili Azam FC walianza kuweka mpira chini na kupunguza kasi ya mchezo huku wakitawala vilivyo katika eneo la kati ya uwanja.
Katika dakika ya 32 Najim Magulu alitumia vyema makosa ya mabeki wa Azam FC kuondosha mpira katika eneo la hatari la kuipatia JKT Ruvu goli lao la kwanza katika mchezo huo wa leo na kupelekea mchezo kwenda mapumziko Azam Fc wakiwa mbele kwa goli 2-1.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku Azam FC wakimpumzihsa Kipre Bolue na nafasi yake ikachukuliwa na Himid Mao.
Katika dakika 59 JKT Ruvu walipoteza nafasi ya wazi ya kujiandikia goli la pili kufuatia washambuliaji wa JKT Ruvu kushindwa kuweka mpira kimiani wakati wamebaki na nyavu na huku wakiwa wa wili dhidi ya beki mmoja wa Azam FC.
Shomari Kapombe katika dakika ya 60 aliangushwa katika eneo la hatari na mwamuzi kizawadia Azam FC penati iliyozaa goli la tatu kwa Azam FC iliyo pigwa na John Bocco.
Kuingi kwa goli hilo Azam FC walijaribu kupunguza kasi ya mchezo kitendo ambacho JKT Ruvu hawakuliwafiki na kuendeleza kasi ya kusaka goli.
Katika dakika ya 69 JKT Ruvu waliandika goli la pili kupitia kwa Emanuel Pius na kupeleka Azam FC kuanza kusaka goli la kumaliza mchezo huku JKT Ruvu wakisaka goli la kusawazisha.
Katika dakika za nyongeza mtokea benchi Kipre Tcheche aliiandikia Azam FC goli la 4 na kupeleka mchezo kumalizika kwa Azam FC wakiibuka na ushindi wa goli 4-2.
Katika ,mchezo mwingine wa ligi kuu ya vodacom uliochezwa katika uwanja wa Sokoine Mbeya Tanzania Prisons wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya African Sports.
Goli hilo pekee la Tanzania Prisons lilifungwa na Said Mkopi kwa mkwaju wa penati katika kipindi cha kwanza.
MATOKEO YA MICHEZO YA LEO
TANZANIA PRISONS 1-0 AFRICAN SPORTJKT RUVU 2-4 AZAM FC
MSIMAMO WA LIGI KUU YA VODACOM BAADA YA MICHEZO YA LEO
Rn | Timu | P | W | D | L | F | A | Gd | Pts |
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
1 | Azam FC | 8 | 7 | 1 | 0 | 15 | 5 | 10 | 22 |
2 | YANGA | 8 | 6 | 2 | 0 | 20 | 5 | 15 | 20 |
3 | MTIBWA SUGAR | 8 | 6 | 1 | 1 | 8 | 4 | 4 | 19 |
4 | SIMBA SC | 8 | 6 | 0 | 2 | 9 | 4 | 5 | 18 |
5 | STAND UNITED | 9 | 5 | 1 | 3 | 10 | 4 | 6 | 16 |
6 | T. PRISONS | 9 | 5 | 1 | 3 | 8 | 8 | 0 | 16 |
7 | MWADUI FC | 9 | 4 | 3 | 2 | 10 | 6 | 4 | 15 |
8 | TOTO AFRICANS | 9 | 3 | 4 | 2 | 6 | 7 | -1 | 13 |
9 | MGAMBO SHOOTING | 9 | 3 | 2 | 4 | 6 | 8 | -2 | 11 |
10 | MAJIMAJI FC | 9 | 3 | 2 | 4 | 5 | 8 | -3 | 11 |
11 | MBEYA CITY | 9 | 2 | 2 | 5 | 7 | 8 | -1 | 8 |
12 | NDANDA FC | 8 | 1 | 4 | 3 | 4 | 6 | -2 | 7 |
13 | Coastal Union | 9 | 1 | 3 | 5 | 1 | 7 | -6 | 6 |
14 | KAGERA SUGAR | 9 | 1 | 2 | 6 | 2 | 11 | -9 | 5 |
15 | AFRICAN SPORT | 8 | 1 | 0 | 7 | 1 | 9 | -8 | 3 |
16 | JKT RUVU | 9 | 0 | 2 | 7 | 4 | 16 | -12 | 2 |
0 Maoni:
Post a Comment