Wednesday, March 2, 2016

MAJARIBIO YA KUJIUNGA NA AZAM ACADEMY YASOGEZWA MBELE

Posted By: Abdallah Sulayman - 6:58 PM

Share

& Comment

Azam FC inapenda kuufahamisha umma kuwa wikiendi hii Jumamosi (Machi 5 mwaka huu) hakutakuwa na majaribio kwa wachezaji wenye umri chini ya miaka 20 (U-20) na wale wa miaka 12 hadi 16.

Majaribio hayo sasa yatafanyika Machi 12 mwaka huu kwenye Makao Makuu yetu Azam Complex, Chamazi, kuanzia saa 1.30 asubuhi kwa wale wenye umri wa kuanzia miaka 12 hadi 16 na saa 8.30 asubuhi kwa wenye chini ya miaka 20.

Kusogezwa mbele kwa majaribio hayo kunatokana na muingiliano wa tarehe hiyo na siku ya mchezo muhimu wa Azam FC wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) dhidi ya Yanga utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Jumamosi hii.

Azam FC inayodhaminiwa na Benki ya NMB imekuwa na utaratibu mzuri wa kuinua na kuibua vipaji vya vijana na kila Jumamosi ya kwanza ya kila mwezi imekuwa ukiendesha zoezi la majaribio kwa vijana chini ya miaka 20 na kila Jumamosi kwa wale walio chini ya miaka 16 (12, 14 na 16).

Imetolewa na Idara ya Ufundi ya Azam FC Academy
Azam FC; 
'Timu Bora, Bidhaa Bora'

1 Maoni:

  1. Aaah mwezi huu unaokuja wa 9 itafanyika lini majaribio

    ReplyDelete

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.