Friday, October 12, 2012

SIMBA NA YANGA KUJA CHAMANZI

Posted By: azam fans - 7:26 PM

Share

& Comment

Uongozi wa Azam FC imetuma barua kwa TFF kuomba mchezo yake ya nyumbani dhidi ya Simba na Yanga ipigwe katika uwanja wa Chamanzi unaomilikiwa na Azam FC.

Azam FC hutumia uwanja wa Taifa kama uwanja wa nyumbani pale wanapocheza na Simba na Yanga na ratiba ya ligi kuu ya Vodacom inaonyesha Azam FC atatumia uwanja wa Taifa kama uwanja wake wa nyumbani pale watakapo kabiliana na timu hizo, ambazo ndizo uwanja wake wa nyumbani.

"Azam imeomba mechi zake za nyumbani dhidi ya Yanga na Simba zichezwe kwenye uwanja wake wa Azam Complex ulioko Chamazi badala ya Uwanja wa Taifa," ilieleza taarifa ya TFF iliyotumwa kwa vyombo vya habari.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa; "Maombi hayo yatawasilishwa kwenye kikao cha Kamati ya Ligi ya TFF kinachotarajiwa kufanyika kesho (Oktoba 13 mwaka huu) kwa ajili ya kufanyiwa uamuzi."


Wakati huo huo kikosi cha Azam FC kipo mkoani Morogoro kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu ya vodacom dhidi ya Polisi Moro utakaochezwa katika uwanja wa Jamuhuri mkoani Morogoro hapo kesho.

1 Maoni:

  1. Hii ni vizuri sana. Ilifaa hata iwe imeshafanywa maana hakuna maana ya kuwa na uwanja lakini mechi za nyumbani zinachezewa ugenini.

    ReplyDelete

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.