Wednesday, July 29, 2015

AZAM WATINGA NUSU FAINALI, WAICHAPA YANGA

Posted By: kj - 7:12 PM

Share

& Comment


Azam FC leo wamefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya kombe la Kagame ikiwa ni mara ya pili kwa Azam FC kutinga katika hatua hiyo katika michuano hiyo mikubwa kwa ukanda huu wa Afrika Mashariki na kati.

Azam FC leo waliwakabili Yanga SC katika mchezo wa robo fainali ya nne ya kombe la Kagame na dakika 90 kumalizika kwa sare ya bila kufungana kuchukuliwa changamoto ya mikwaju ya penati ambayo imewaondosha yanga.

Katika mchezo wa leo dakiak 15 za mwanzo Azam FC waliutawala mchezo na kutengeneza nafasi mbili za kujipatia goli lakini walishindwa kuzitumia.

Baada ya dakika 15 yanga SC walianza nao kutengeneza nafasi huku wakitala mchezo kwa kupokezana na Azam FC na mpaka dakika 45 za mwanzo zinakwisha Azam FC 0 na Yanga SC0.

Kipindi cha pili Azam FC walianza kwa mabadilko kwa kumpumzisha beki chipukizi Abdallah Kheri na Franky Domayo na kuingia Said Morad na Ame Ally.

Katika kipindi cha pili Ynaga Sc walionekana kuwa na hatari zaidi ya Azam Fc huku wakishambuliana kwa zamu.

Yanga Sc pia walifanya mabadiliko ya kumtoa Jum Abdul aliyeumia, Deus Kaseke na Haruna Niyonzima na nafasi zao kuchukuliza na Zottah, Salim Telela na Malim Busungu mabadiliko ambayo hayakubadili ubao wa magoli na kupelekea mchezo kumalizika kwa sare ya bila kufungana.

Baada ya dakika 90 kumalizika mikwaju ya penati ikachukuwa hatua ambapo Azam FC walishinda mikwaju yote mitano na yanga kupoteza penati moja na kupelekea matokeo kusomeka 5-3.

Kwa ushindi huo wa leo Azam FC itacheza na KCCA ya Uganda katika mchezo wa nusu fainali ya pili siku ya ijumaa katika uwanja wa Taifa

Penati za Azam FC zilipigwa na Kipre Tcheche, John Bocco, Himid Mao, Pascal Wawa na Aggrey Morice.

Penati za Yanga zilipigwa na Salim Telela, Nadir Haroub na Geofrey Mshuiya huku Mwinyi Hajji akikosa penati.

Kikosi cha Azam FC leo: Aishi Manula, Aggrey Morice, Pascal Wawa, Abdallah Kheri/Said Morad, Shomari Kapombe, Himid Mao, Farid Mussa Malik, Jean Mugeraniza, Frank Domayo/Ame  Ally, John Bocco na Kipre Tcheche.

Kikosi cha yanga sc leo:Ali Mustafa, Juma Abdul/Joseph Zuttah,Haji Mwinyi, Kelvin Yondani, Nadir Ali, Mbuyu Twite,Deusi Kaseke/Salumu Telela, Haruna Niyonzima/Malimi Busungu, Amisi Tambwe, Donald Ngoma, Geoffrey Mwashuiya

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.