Friday, July 31, 2015

FARID MUSSA AIPELEKA AZAM FC FAINALI

Posted By: kj - 6:00 PM

Share

& Comment

Kiungo chipukizi wa Azam FC, Farid Mussa Shah ameipeleka Azam FC katika fainali ya michuano ya kombe la kagame baada ya kuifungia goli pekee katika mchezo wa nusu fainali ya pili dhidi ya KCCA ya Uganda.

Katika mchezo huo wa leo ulioanza saa tisa na dakika 45 katika uwanja wa taifa, Azam FC waliuwanza mchezo taratibu huku wakiwasoma wapinzani wao KCCA.


Kipindi cha kwanza KCCA walianza na mabadiliko kwa kumpumzisha Mudathir Yahya na nafasi yake kuchukuliwa na Ame Ally Zungu, mabadilko yaliyo izidisha kasi ya Azam FC.



Katika dakika ya 60 Shomari Kapombe aliingia kuchukuwa nafasi ya Erasto Nyoni kitendo kilicho pelekea ufanisi zaidi katyika upande wa kulia wa Azam FC.

Mabadiliko mawaili hayo yaliyo fanywa na kocha Stewart John Hall zilihusika katika goli pekee la Azam FC katika mchezo wa leo, ambapo Kapombe alimpasia Ame na Ame akamtengenezea nafasi Farid Mussa Malik Shah na kuiandika Azam FC goli katika dakika ya 77.


Kuingia kwa goli hilo kuliwatuliza zaidi Azam FC na kucheza soka la uwakika huku wakiimarisha ngome yao na kupelekea mchezo kumalizika kwa Azam FC kuibuka na ushindi wa goli 1-0.


Ushindi huo unaifanya Azam FC kwa mara ya pili kufanikiwa kucheza mchezo wa fainali ya kombe la Kagame, ambapo siku ya jumapili watakuwa na kibarua mbele ya Gor mahia ya Kenya.

MUDATHIR YAHYA KAZINI
FARID MUSSA MALIKI 

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.