Sunday, February 23, 2014

AZAM WATOA SARE NA PRISONS

Posted By: kj - 8:10 PM

Share

& Comment

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgd3ngkqv7XHtm432NCO1wqysHSbBuuXv0r8TOXj9U7DCtiGbZwOUuNOQXN25d-5EqPllljyGyfKLmA8OuUrwE-XB7dMr4N-SsbcCxeu4_DOiublMFmIRMyedVgljoctqMuUcosH5XhXCc/s1600/BOCCO.jpg
Azam FC leo wameshindwa kuomdoka na pointi zote tatu kutoka kwa Tanzania Prizons ya Mbeya baada ya kulazimshwa sare ya goli 2-2 katika mchezo wa ligi kuu ya vodacom uliochezwa katika uwanja wa Azam Complex uliopo Chamanzi.

Katika mchezo huo ambao ulimshuhudia nahodha wa Azam FC John Raphael Bocco akicheza mchezo wake wa kwanza wa Ligi kuu ya vodacom tangu mzunguko wa pili uwanze.

Mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika kulikuwa hakuna timu zilizo ona nyavu za wapinzanmi wake, na hivyo kupelekea magoli yote manne kutiwa kimiani katiki kipindi cha pili.

Tanzania Prisons walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Omega Seme katika dakika ya 47 kwa shuti la mpira wa adhabu baada ya Aggrey Morris kumchezea rafu Jimmy Shoji.

Dakika tatu baadae Aggrey Morris aliisawazishia Azam FC ikiwa ni dakika ya 50 kwa kichwa baada ya kuuwahi mpira uliorudishwa na beki wa Prisons kufuatia John Bocco kuunganisha kwa kichwa mpira wa adhabu wa Erasto Nyoni.

Azam FC walionekana kuwa katika nafasi ya kuondoka na pointi tatu baada ya Kipre Herman Tchetche kuifungia bao la pili timu hiyo dakika ya 51 kwa shuti kali baada ya kuiwahi pasi ndefu ya Nyoni.

Hata hivyo, zikiwa zimesalia dakika mbili mchezo huo kumalizika, Laurian Mpalile aliisawazishia Prisons dakika ya 88 baada ya pasi nzuri ya Freddy Chudu. 

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © 2025 CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.